NAFASI ZA KAZI UTUMISHI WA UMMA FEB 2014
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI
WA
UMMA
Kumb.
Na EA.7/96/01/E/34 17 Februari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA
KAZI
Sekretariati
ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa
Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria
Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki kimepewa
jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa
niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 517 za kazi kwa waajiri
mbalimbali kama ifuatavyo:
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu
tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu
tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro,
Katibu tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa
Njombe.
Waajiri
wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya
ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Msalala.
Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya
ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa
Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe
katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa kwa sharti
hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji
wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V)
yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na
vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha
sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa
kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer Certificate
-
Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
“Transcripts”, “Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji
wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Machi,
2014
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na
NECTA).
xv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
xvi.
Pamoja na waombaji kuainisha waajiri,
Sekretarieti ya Ajira baada ya usaili itawapangia waombaji waliofaulu, kwa
mwajiri yoyote bila kujali chaguo la mwombaji.Hii ni kutokana na baadhi ya
waombaji kupendelea kufanya kazi kwenye baadhi ya maeneo tu.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya Ajira katika
|
|
Public Service
Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
1.0
AFISA LISHE II (NUTRITION OFFICER II) – NAFASI 21
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka
kwa wadau na makundi mbalimbali na kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi
ya wilaya.
·
Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa
ya watoto na makundi mengine yenye lishe duni.
·
Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya
lishe katika ngazi ya wilaya.
·
Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya
lishe katika ngazi ya wilaya.
·
Kusimamia kazi za lishe katika wilaya
·
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu
wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
· Kuajriwa wenye Shahada ya
kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi na Chakula na Teknolojia ya
Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and
Technology and Food Science) au Stashahada ya juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition)
kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
2.0
MSAIDIZI LISHE (NUTRITION ASSISTANT) – NAFASI 16
2.1
KAZI NA MAJUKUMU
·
Kutambua na kuorodhesha na kuweka kumbukumbu
za watoto chini ya miaka mitano na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni
ngazi ya kijiji na kata.
·
Kufuatilia na kutoa ushauri wa lishe kwa kaya
zenye watoto wenye lishe duni.
·
Kuelekeza watoto na makundi mengine yanayoathiriwa
na lishe duni wapelekwe kwenye kituo cha afya Kwa huduma zaidi.
·
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu
huduma za lishe zinazotolewa kwa makundi mbalimbali kwenye kata/kijiji.
·
Kukusanya taarifa na takwimu za lishe katika
sehemu yake ya kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye cheti cha miaka miwili cha mafunzo ya
lishe kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS A kwa mwezi
3.0
MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT)– NAFASI
12
3.1
KAZI NA MAJUKUMU
·
Kulea watoto katika vituo vya malezi ya awali
ya watoto wadogo mchana.
·
Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi
bora ya awali ya watoto wadogo wenye umri wa miaka 0-8.
·
Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya
watoto vijijini/sehemu au eneo la vituo.
·
Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya
watoto wadogo.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha nne waliofaulu mafunzo ya mwaka mmoja ya malezi ya awali ya watoto wadogo
wenye umri kati ya miaka 0-8 kutoka katika Chuo kinachotambulika na serikali au
wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo ya ustawi wa jamii.
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS B Kwa mwezi
4.0
AFISA USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE OFFICER II)–
NAFASI 184
4.1
KAZI NA MAJUKUMU
·
Kuendesha usaili kwa wahudumiwa (watu wenye
ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, pamoja na watoto na vijana wenye
matatizo mbalimbali).
·
Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi
wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili.
·
Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa
mazingira ya wahudumiwa.
·
Kupokea na kukusanya taarifa za ustawi wa
jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya ustawi wa jamii.
·
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu
huduma za watu wenye ulemavu, wazee malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
·
Kupokea kuchambua na kuandaa orodha ya maombi
ya uandikishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ambao (foster
care) na vyuo vya malezi vya watoto wadogo mchana.
·
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya
maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama waliojifungua watoto watatu au
zaidi kwa mara moja.
·
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya
maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali.
·
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi
mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
·
Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa.
·
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu
wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
B.A (social work or sociology) au stashada ya juu ya Ustawi wa jamii (Advanced
Diploma in Sociol work) kutoka chuo cha juu kinachotambuliwa na ustawii wa
jamii.
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
5.0
MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II
(SOCIAL WELFARE ASSISTANT II) – NAFASI 24
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutambua na kuhudumia watu walio katika
makundi maalum na mazingira hatarishi.
·
Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio
katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
·
Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi
mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
·
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu
wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali TGS C kwa mwezi.
6.0
MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II (KITCHEN/MESS
ATTENDANT)
–
NAFASI 4
6.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusafisha Vyombo vya kupikia.
·
Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.
·
Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.
·
Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya
Mpishi na Mezani.
·
Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.
·
Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha Nne.
6.3
MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
7.0
AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) –
NAFASI 6
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na
misitu.
·
Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa
isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
·
Kufanya
utafiti wa misitu.
·
Kutekeleza
Sera na Sheria za misitu.
·
Kuendesha
mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
·
Kukusanya
takwimu za misitu.
·
Kufanya
ukaguzi wa misitu.
·
Kupanga
na kupima madaraja ya mbao.
·
Kudhibiti
leseni na uvunaji wa miti.
·
Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya
uendelezaji na matumizi endelevu ya miti kwa wananchi.
·
Kufanya
ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
·
Kupima
maeneo na kuchora ramani za misitu.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo
Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
8.0
MSAIDIZI MISITU DARAJA LA II (FORESTRY
ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 75
8.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukusanya mbegu
·
Kuhudumia
na kutunza bustani za miti.
·
Kutunza
na kuhudumia miti na misitu.
·
Kufanya
doria.
·
Kusimamia
ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
·
Kukusanya
takwimu za misitu.
·
Kusimamia
kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.
·
Kukusanya
maduhuli.
·
Kupima
mazao ya misitu.
·
Kufanya
doria.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Kidato
cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Misitu
kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C kwa mwezi.
9.0
MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURE GENERAL) –
NAFASI 10
9.1
KAZI NA MAJUKUMU
·
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo
na kuitafsiri kwenye masomo.
·
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo
(lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kufundisha
kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
·
Kuandaana
kufundisha kozi za Wakulima.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practical).
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
9.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
· Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agriculture General)
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
10.0
MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRONOMY) – NAFASI 4
10.1 KAZI NA MAJUKUMU
·
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo
na kuitafsiri kwenye masomo.
·
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo
(lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kufundisha
kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
·
Kuandaana
kufundisha kozi za Wakulima.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practical).
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
10.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
· Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agronomy) kutoka
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali,
waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
11.0
MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HORTICULTURE) – NAFASI 1
11.1 KAZI NA MAJUKUMU
·
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo
na kuitafsiri kwenye masomo.
·
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo
(lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kuandaana
kufundisha kozi za Wakulima.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practical).
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
11.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
· Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Horticulture) kutoka Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali,
waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
12.0
MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HUMAN NUTRITION) – NAFASI 1
12.1 KAZI NA MAJUKUMU
·
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo
na kuitafsiri kwenye masomo.
·
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo
(lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kufundisha
kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
·
Kuandaana
kufundisha kozi za Wakulima.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practical).
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
12.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor
of Human Nutrition) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za
kufundishia (Teaching Methodology)
12.3 MSHAHARA
13.0
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO –
OFFICERS) – NAFASI 71 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27
NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki
na kila mwezi,
·
Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao
katika masoko kila wiki/kila mwezi,
·
Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
·
Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya
pembejeo na zana,
·
Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya
biashara,
·
Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya
udongo na maji,
·
Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa
wadau,
·
Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa
sekta ndogo ya mazao,
·
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji
mboga, matunda, maua na mazao mengine,
·
Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu
bora,
·
Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza
mbegu bora,
·
Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
·
Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa
kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,
·
Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga,
matunda, maua na viungo,
·
Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
·
Kufanya utafiti mdogo wa mazao yanayofaa
kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,
·
Kufanya utafiti wa udongo,
·
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya
wakulima/wamwagiliaji,
·
Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa
na watafiti,
·
Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio
vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika
mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
14.0
MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO –
ENGINEERS) – NAFASI 38 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE
27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima
kutumia zana za kilimo,
·
Kushiriki katika kufundisha wakulima na
matumizi bora ya zana,
·
Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za
umwagiliaji,
·
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya
umwagiliaji,
·
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha
wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
·
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
·
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za
umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,
·
Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za
za kilimo,
·
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama
kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
·
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora
na
·
Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri
waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
Serikali.
14.3 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
15.1 MUUNDA
BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE
WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI
YAO BADO YANACHAMBULIWA.
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusaidia kuunda boti za uvuvi
·
Kuwashauri
wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
·
Kufanya
matengenezo ya boti.
·
Kusaidia
kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
·
Kuandaa
vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye stashahadaya Uundaji boti
kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS C kwa mwezi
16.1
DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY /
BOAT OPERATOR) – NAFASI 1 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA
TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufunga na kufungua kamba za kivuko.
·
Kuchunga
usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.
·
Kupanga
abiria au magari kwenye kivuko.
·
Kuendesha
na kuongoza kivuko.
·
Kutunza
daftari za safari ya kivuko.
·
Kuhakikisha
kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
·
Kuangalia
mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
16.1 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza
Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au
Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka
miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini,
kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.
16.2 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
17.1 AFISA
MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 8 (LINARUDIWA). KWA WALE
WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA
MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo
wilayani.
·
Ataratibu
uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
·
Atasaidia
kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
·
Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji
bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
·
Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya
masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.
·
Atabuni,
kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
·
Atafanya soroveya ya rasilimali (resource
survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la
kazi.
·
Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na
wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
·
Atatafiti
maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
·
Atafanya
utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
·
Atashiriki katika shughuli za kudhibiti
milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
·
Ataandaa
taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
·
Atafuatilia,
kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
·
Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani
yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo(Animal
Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana
nayo.
17.3 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS D kwa mwezi
18.1 MHASIBU
MSAIDIZI (ASSISTANT ACCOUNTANT) - NAFASI 3 18.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kupokea na kulipa fedha.
·
Kutunza
daftari ya fedha.
·
Kufanya
usuluhisho wa hesabu za benki
·
Kukagua hati za malipo.
·
Kupitisha
malipo kulingana na kanuni za fedha.
·
Kusimamia
kazi za wasaidizi wa hesabu.
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Cheti cha kufaulu mtihani
mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher Standard Government Accountancy
Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma. Au
·
Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya
uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyyote inayotambuliwa na serikali.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi
19.0
AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE
OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
19.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi
vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture )
·
Kuhamasisha
uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
·
Kukusanya
na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
·
Kutoa
ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
·
Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika
Shirikishi katika vyama vya ushirika vya Msingi.
19.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au
Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani ya Ushirika (Cooperative
management and accounting) kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
19.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
20.0
AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
20.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa
makisio ya vifaa vinavyohitajika (Material Requirement Budget) na Mpango wa
Ununuzi (Procurement Plan).
·
Kukusanya
na kutunza takwimu za utendaji za Wazabuni mbalimbali.
·
Kukusanya
na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.
·
Kusimamia
utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
·
Kusimamia
upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).
·
Mfumo
wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).
·
Kusimamia ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa
mara (Perpetual Stock Checking) ghalani.
·
Kutayarisha
Taarifa za kazi katika vipindi maalumu.
·
Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa
vilivyomo ghalani kila mwisho wa mwaka (Annual Stock Taking).
·
Kufanya
kazi zingine ambazo atapangiwa.
20.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara (B.Comm)
yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in
Materials Management) inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya
usimamizi wa Vifaa.
20.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS D mwezi.
21.0
AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) –
NAFASI 1
21.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
·
Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na
wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji
kutunzwa kabla ya kufutwa.
·
Kufungua
na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
·
Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu
ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
·
Kutoa
vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
·
Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo
vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.
·
Kuandaa
hati za kupokelea vifaa.
·
Kufanya
kazi zingine atakazopangiwa.
21.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye cheti cha “National
Store-Keeping Certificate au “Foundation Certificate” kitolewacho na Bodi ya
Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bäodi ya Taifa
ya Usimamizi wa Vifaa.
AU
·
Kuajiriwa wenye Diploma ya Kawaida “Ordinary
Diploma in Materials Management” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa
ya Usimamizi wa
Vifaa.
21.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.A na B kwa mwezi.
22.0
AFISA UTAMADUNI II (CULTURAL OFFICER GRRADE II) – NAFASI
1
22.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutafiti masuala ya Lugha, Sanaa, Mila na
Desturi katika ngazi ya Wilaya.
·
Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni
katika Vyuo na Vituo vya Elimu na mafunzo ya utamaduni.
·
Kazi
nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.
22.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye shahada au stashahada ya juu katika Sanaa, Lugha au Sayansi ya Jamii na
uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
22.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
23.0
AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II
(YOUTH DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
23.1
MAJUKUMU
YA KAZI
·
Kuratibu na
kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana
·
Kuratibu
shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana
·
Kuhamasisha
vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini
·
Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi
za maisha, stadi za kazi na Afya ya Vijana
·
Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa
Vijana na Elimu ya Familia kwa kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali
(NGO)
·
Kukusanya
takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana
·
Kuratibu
shughuli mbalimbali za NGO
zinazoshughulikia masuala ya Vijana
·
Kuandaa
mipango ya kuboresha malezi ya Vijana
·
Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali
wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali
·
Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali
walivyonavyo Vijana ili kuwawezesha kujiajiri
·
Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili
kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiajiri.
23.2
SIFA
ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (BA. in
Sociology or Social Sciences) au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii au
Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya Vijana (Advanced Diploma in Social Works or
Community Development or Youth Development) kutoka chuo kinachotambuliwa na
Serkali.
23.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS D kwa mwezi.
24.0
AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II
(BEEKEEPING OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
24.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na
manzuki.
·
Kutangaza
Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
·
Kukusanya
takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
·
Kupanga
na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
24.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya
Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
24.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
25.0
AFISA ARDHI DARAJA LA II (LAND OFFICER GRADE II) – NAFASI
1
25.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika
kompyuta.
·
Kushughulikia
utayarishaji wa nyaraka za kisheria.
·
Kufanya
ukaguzi wa viwanja.
·
Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa
miliki kwa visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria.
·
Kuwasiliana
na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.
25.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu
katika fani ya Usimamizi ardhi na Uthamini au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo
Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua
miaka mitano.
25.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
26.0
FUNDI SANIFU DARAJA LA II - KOMPYUTA
(COMPUTER TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 1
26.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa
kazi
26.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo
ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani
yenye muelekeo wa kompyuta
·
Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya
ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali
katika fani ya kompyuta
·
Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya
I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
·
Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani yenye
muelekeo wa kompyuta katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
26.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS C kwa mwezi
27.0
AFISA BIASHARA DARAJA LA II (TRADE OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
27.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuwasiliana na Wizara nyingine ambazo
zinafanya biashara, kupata takwimu ambazo zitatumika katika kutathimini
mwenendo wa biashara na masuala mengine ya kibiashara.
·
Kusambaza
taarifa za kibiashara kwa wafanyabiashara.
·
Kutathmini mwenendo wa biashara kwa kuangalia
hali ya masoko katika nchi mbalimbali ambazo bidhaa zetu zinauzwa.
·
Kuandaa grafu na “chart” ambazo zinaonyesha,
mwenendo wa bidhaa zinazoingizwa nchini na zile ziendazo nje kwa kila nchi
ambazo hufanya biashara na Tanzania.
27.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya
Biashara waliojiimarisha katika fani ya Uchumi, Masoko, Uendeshaji Biashara au
inayolingana nayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam au chuo kingine chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
27.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
28.0
MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 1
28.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandika na kutunza “register” zinazohusu
shughuli za uhasibu.
·
Kuandika
hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
·
Kutunza
majalada yenye kumbukumbu za hesabu
·
Kupeleka
barua/nyaraka za uhasibu Benki.
·
Kufanya
usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
28.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au
“Foundation Level” kinachotolewa na
NBAA
28.3
MSHAHARA
29.0
AFISA USIMAMIZI WA FEDHA DARAJA LA II
(FINANCE MANAGEMENT OFFICER II) - NAFASI 1
29.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities)
za Serikali.
·
Kufuatilia
hati za hisa.
·
Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu
maendeleo ya utekelezaji wa miradi.
·
Kuweka
kumbukumbu za madeni ya nje.
·
Kuweka
kumbukumbu za mikopo ya ndani.
·
Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya
makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali.
·
Kufuatilia
utayarishaji na uchambuzi wa “Flash Reports” za kila mwezi.
29.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya Uchumi na Mipango (Major in Economics) au
Biashara au Sheria (LL.B) au Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Uchumi &
Mipango au Biashara au Stashahada ya juu ya Usimamizi wa kodi kutoka
Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
·
Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu
CPA (T) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA
watafikiriwa kwanza.
29.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
30.0
AFISA TARAFA – NAFASI 6
30.1
MAJUKUMU YA KAZI
(i)
Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
·
Kumwakilisha
na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu
katika Tarafa.
·
Kuandaa
na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata
kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
·
Kuhamasisha
na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
·
Kuwa
kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
·
Kuwa
mlinzi wa amani katika eneo lake.
·
Kufuatilia
na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha
kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
·
Kuratibu
shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
·
Kuandaa
taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za
maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
·
Kufanya
kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii)
Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
·
Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa
katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
·
Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa
Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
·
Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa
mipango ya Maendeleo katika eneo lake
·
Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na
Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
·
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika
eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
·
Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za
Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
30.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu
katika mojawapo ya fani za Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo,
Mifugo,Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
30.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
31.0
AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER
GRADE II)
–
NAFASI 1
31.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa
vyuo, shule, na vituo vya Elimu na Mafunzo
·
Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa
waalimu, Makocha, viongozi wa vyama na vilabu vya michezo
·
Kufundisha
fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
31.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu
ya Elimu ya Michezo (Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na
Serikali.
31.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS D kwa mwezi.
32.0
FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI
(TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING) –
NAFASI 1
32.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushughulikia madaai/malalamiko ya hati za
viwanja, kuweka na kutunza kumbukumbu zake
·
Kutunza
kumbukumbu za “cadastrals surveys” na mahesabu yake
·
Kuandaa
nakala za “cadastral site plans”
·
Kutunza
miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
32.2
SIFA
ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye wahitimu wa kidato cha nne au
sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani
(Mapping)
32.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS C kwa mwezi.
33.1
FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) –
NAFASI
1
33.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya maandalizi ya Uchoraji wa ramani za
miji kadiri ya uwiano unaohitajika
·
Kutunza
kumbukumbu za ramani na plan
·
Kuchora
plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji
·
Kutoa
nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji
33.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha
sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili au Stashahada katika
fani ya Urasimu Ramani (Cartography) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na
serikali.
33.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS C kwa mwezi
34.1
FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI -
(TECHNICIAN GRADE II - WATER) – NAFASI 1
34.1
MAJUKUMU
YA KAZI
·
Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
·
Kutunza
takwimu za maji
·
Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H:
12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro
·
Kuchora
hydrograph za maji
·
Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za
winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k.
·
Kufanya
matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia
maji na hali ya hewa
·
Kuingiza
takwimu kwenye kompyuta
34.2
SIFA
ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi
vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada
ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
34.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS C kwa mwezi
35.1
AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 1
35.1
MAJUKUMU
YA KAZI
·
Kutekeleza Kazi za Ushirikishaji Wadau Katika
Uhifadhi.
·
Kudhibiti Utoaji wa Leseni za Biashara Za
Nyara na Vibari vya Kukamata Wanyama Hai.
·
Kushiriki
Katika Kusuluhisha Migogoro ya Matumizi ya Wanyamapori
·
Kudhibiti Matumizi Haramu ya Leseni za
Uwindaji na Kuhahakikisha Kufuatwa Kwa Maadili Katika Kutumia Wanyamapori.
·
Kuthibiti
Matumizi Haramu ya Wanyamapori.
·
Kufuatilia
Utekelezaji wa Miongozo Mbalimbali ya Uhifadhi Wanyamapori.
·
Kuhakiki
Viwango vya Kukamata Wanyama Hai Kwa Ajili ya Biashara na Ufugaji.
·
Kufanya
Kazi za Kuzuia Ujangili.
·
Kukusanya
Taarifa, na Takwimu za Uhifadhi.
·
Kutekeleza
Kazi za Uhifadhi Katika Mapori ya Akiba.
35.2
SIFA
ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa Wenye Shahada ya Sayansi ya
Wanyamapori Kutoka Chuo Kikuu Kinachotambuliwa na Serikali.
35.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS D kwa mwezi
36.1
AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) –
NAFASI 2
36.1
MAJUKUMU
YA KAZI
Hili
ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili
watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa
ni pamoja na:
·
Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria
pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
·
Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu
masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za
juu.
36.2
SIFA
ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili
yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
36.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS E kwa mwezi
X. M. Daudi
Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma.
Post a Comment