Header

NAFASI ZA KAZI UHAMIAJI FEB 2014

Kamishna Mkuu wa idara ya Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji . Nafasi hizo ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji , Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji .

MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIANI ( NAFASI 70 )
SIFA ZINAZOHITAJIKA

Awe na shahada ya Kwanza au stashahada ya juu katika vyuo vinavyotambulika na serikali katika fani zifuatazo ;
Sheria , Uchumi , Biashara , Utawala , Uandishi wa Habari , Uhalimu , Usafirishaji , Rasilimali Watu , Sayansi ya Kompyuta , Teknologia ya Habari na Mawasiliano , Takwimu , Uchapaji , Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo .

Umri usizidi Miaka 35

KOPLO WA UHAMIAJI ( NAFASI 100 )
SIFA ZINAZOHITAJIKA

j. Awe amehitìmu Kidato cha sita na kufaulu.
ii. Umri usiozidi miaka thelathini(30).

KONTEBO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)
SIFA ZINAZOHITAJIKA

j. Awe amehitìmu Kidato cha nne na kufaulu.
ii. Umri usiozidi miaka (25).

A: MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kulùngua, kupanga na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa huduma
za Uhamiaji.
(ii) Kuandika Hati mbalímbaLi za Ubamiaji
(iii) Kufanya Doria schcme za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, treni na sehemu zenye
vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwcmo vya majini.
(iv) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni
wanaofukuzwa nchini (Deporters).
Kufanya ukaguzi kwcnye mahoteli, nyumba za kulaLa wageni na sehemu za biashara.
(vi) Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila
siku za Uhamiaji.
(vii)Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji.

C: SIFA ZA ZIADA
(I) Ujuzi na elimu ya kompyuta na uandishi mzuri utazingatiwa.
(ii) Cheti cha ufundi stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya umeme na mitambo.
(iii) Mwenye cheti au Stashahada ya Uhazili (Certificate or Diploma in Secretarial Studies)
katika chuo kinachotambulika na Serikalì.
(iv) Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statistics) kutoka Chito cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Statistical Training Centre) au chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Cheti au Stashahadayavyombo vyaMajini (Certificate orDiploma in Marine Transportation
and Operation) kutoka katika Chuo cha Bandan (Dar es Salaam Marine Institute) au Chuo
kinachotambulika na Serikali.
(vi) Lcseni ya gari Daraja “C”, cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II pamoja na cheti cha
mafunzo ya Juu ya Udereva wa magari Daraja la IL (Advanced Drivers Course Grade 11)
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(vii) Mwombaji atafikiriwa zaidi endapo atakuwa na uzoefu wa kazi za kiuhamiaji.

D: UWASILISHAJI WA MAOMBI
Barua ya maombi ziainbatanishwe na:
(I) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masonia kwa mujibu wa sifa zilizotajwa.
(ii) Nakala ya “Leaving Certificate”
(iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
(iv) Picha mbili (passport size)
Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa.
(vi) Maombi yapitie posta na barua ziandikwe kwa mkono.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

MAOMBI YA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI UHAMIAJI YATUMWE

KATIBU MKUU ,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ,
S.L. P 9223,
DAR ES SALAAM.

MAOMBI YA NAFASI YA KOPLO WA UHAMIAJI NA KONSTEBO WA UHAMIAJI YATUMWE KWA 

KAMISHINA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L. P 512,
DAR ES SALAAM.

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 27/02/2014.

Source: gazeti la mwananchi Ijumaa , 14 , 2015 , mtanzania Ijumaa , 14 , 2015

Tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya Idara ya Uhamiaji na wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi .