Header

Afisa Usalama Maji

NAFASI # 2: Afisa Usalama Maji- Nafasi 1.
Habari:
Community Forests Pemba(CFP) inahitaji; Afisa Usalama wa Maji ili kusaidia Jumuiya katika shughuli za uvunaji wa maji ya mvua. Pamoja na kazi hiyo, Afisa Usalama wa Maji atakuwa na wajibu wa kufanyakazi za uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa jamii (Water catchment conservation) kwa kushirikiana na afisa misitu, kilimo mseto na wataalam wengine.

Sifa za muombaji:
1. Awe na Stashahada au shahada kutoka taasisi inayotambuliwa katika fani ya uvunaji wa maji ya mua pamoja na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kwenye ujuzi huo na maendeleo ya jamii
Awe na ujuzi wa hali ya juu katika kufundisha na Mawasiliano

Majukumu:
• Kubuni na kutekeleza mifumo ya uvunaji wa maji ya mvua
• Awe na mbinu mbali mbali za uvunaji wa maji ya mvua ni pamoja na ferrocement technique.
• Kutekeleza mifumo ya kuchuja maji ya mvua
• Kuendeleza na kutekeleza kazi za hifadhi ya vyanzo vya maji kwa kushirikiana na vitengo vyengine.
• Kufuatilia maendeleo ya mradi na ubora wa maji.
• Ukusanyaji na uwekaji wa takwimu za mradi.
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.

Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja.


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Barua ya maombi yanatakiwa yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza pamoja na CV ya muombaji, na nakala za vyeti vyake.

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Mei saa 11:30 asubuhi. Wanawake wenye sifa watapewa kipaumbele.
Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa mkono, kwa posta au kwa barua pepe kwenda anuani iliopo hapo chin:-
Mkurugenzi Mtendaji
Community Forests Pemba (CFP)
P.O. Box 177, Wete-Pemba
Minyenyeni – Pemba