Header

Afisa wa Nishati Mbadala

Nafasi # 3: Afisa wa Nishati Mbadala- Nafasi 1.
Habari:
Community Forests Pemba inahitaji, Afisa wa Nishati Mbadala ili kusaidia Jumuiya katika kazi za nishati ya jua. Aidha, Afisa Nishati Mbadala atatakiwa kusaidia na kutoa taaluma utengenzaji na matumizi ya mkaa wa kisasa utokanao na mabaki ya organic products(briquette) na kuanziasha kazi za uboresheji wa uzalishaji mkaa.

Sifa za muombaji:
1. Awe na Stashahada au shahada kutoka taasisi inayotambuliwa katika fani husika.
2. Awe na uzoefu wa miaka mitatu katika fani hiyo na maendeleo ya jamii
3. Awe na ujuzi wa hali ya juu katika kufundisha na Mawasiliano

Majukumu:
• Kubuni na kutekeleza mifumo ya nishati ya jua katika vijiji husika
• Kufundisha jamii husika juu ya mfumo utakaowekwa na matumizi yake
• Kutoa taaluma ya utengenezaji wa majiko sanifu
• Kufanya majaribio ya mifumo bora ya uzalishaji wa mkaa.
Kufuatilia maendeleo ya mradi
• Ukusanyaji na uwekaji wa takwimu za mradi.
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.
Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Barua ya maombi yanatakiwa yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza pamoja na CV ya muombaji, na nakala za vyeti vyake.

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Mei saa 11:30 asubuhi. Wanawake wenye sifa watapewa kipaumbele.
Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa mkono, kwa posta au kwa barua pepe kwenda anuani iliopo hapo chin:-
Mkurugenzi Mtendaji
Community Forests Pemba (CFP)
P.O. Box 177, Wete-Pemba
Minyenyeni – Pemba