Header

NAFASI ZA KAZI - Community Forests Pemba (CFP)

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Community Forests Pemba (CFP) inatangaza nafasi za kazi zifuatazo:-
Nafasi # 1. Forestry Office- Nafasi 1.
Community forests Pemba(CFP) inahitaji Forests Officer kwa ajili ya kuisaidia Jumuiya kwenye kazi za uanziashaji wa misitu vijijini pamoja na uhifadhi wa misitu ya asili,Katika nafasi hiyo forests Officer atatakiwa kushirikiana na kushirikiana na kufanikisha kazi  za Agroforestry, Spice Forests production na kazi za Catchment Conservation.
Sifa za Muombaji
Awe amemaliza na kuwa na cheti cha Forestry, katika ngazi ya Diploma au Digrii ya kwanza au fani nyengineo yenye kufanana kutoka kwenye chuo chenye kutambulika ndani na nje ya nchi.
Awe na uzowefu wa kazi na ujuzi usiopungua Miaka mitatu katika fani ya  misitu na maendeleo ya jamii
Awe na ujuzi wa hali ya juu katika kufundisha na Mawasiliano

• Kuanzisha vitalu vya miti ya jamii
• Kutoa mafunzo ya ugani
• Kutoa msaada wa upandaji miti kwa jamii
• Kuendeleza mipango ya usimamizi wa misitu kwenye misitu ya jamii na mashamba makubwa
• Kufuatilia ukuaji na maendeleo ya mradi
• Ukusanyaji wa takwimu za mradi atakaofanyia kazi
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.

Nafasi hii itaanza rasmi 1 Agosti 2015

NAFASI  # 2: Afisa Usalama Maji- Nafasi 1.
Habari:
Community Forests Pemba(CFP) inahitaji;  Afisa Usalama wa Maji ili kusaidia  Jumuiya katika  shughuli za uvunaji wa  maji ya mvua. Pamoja na kazi hiyo, Afisa Usalama wa Maji atakuwa na wajibu wa kufanyakazi za uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa jamii (Water catchment conservation)  kwa kushirikiana na afisa  misitu, kilimo  mseto na wataalam wengine.
Sifa za muombaji:
1. Awe na Stashahada au shahada kutoka taasisi inayotambuliwa katika fani ya uvunaji wa maji ya mua pamoja na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kwenye ujuzi huo na maendeleo ya jamii
Awe na ujuzi wa hali ya juu katika kufundisha na Mawasiliano
Majukumu:
• Kubuni na kutekeleza mifumo ya uvunaji wa  maji ya mvua
• Awe na mbinu mbali mbali za uvunaji wa maji ya mvua ni pamoja na ferrocement technique.
• Kutekeleza mifumo ya kuchuja maji ya mvua
• Kuendeleza na kutekeleza kazi za hifadhi ya vyanzo vya maji kwa kushirikiana na vitengo vyengine.
• Kufuatilia maendeleo ya  mradi na ubora wa maji.
• Ukusanyaji na uwekaji wa takwimu za mradi.
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.

Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja.

Nafasi # 3: Afisa wa Nishati Mbadala- Nafasi 1.
Habari:
Community Forests Pemba inahitaji, Afisa  wa Nishati Mbadala ili kusaidia Jumuiya katika kazi za nishati ya jua. Aidha, Afisa Nishati Mbadala atatakiwa kusaidia na kutoa taaluma utengenzaji na matumizi ya mkaa wa kisasa utokanao na mabaki ya organic products(briquette) na kuanziasha kazi za uboresheji wa uzalishaji mkaa.
Sifa za muombaji:
1. Awe na Stashahada au shahada kutoka taasisi inayotambuliwa katika  fani husika.
2.  Awe na uzoefu wa miaka mitatu katika fani hiyo  na maendeleo ya jamii
3. Awe na ujuzi wa hali ya juu katika kufundisha na Mawasiliano
Majukumu:
• Kubuni na kutekeleza mifumo ya nishati ya jua katika vijiji husika
• Kufundisha  jamii husika juu ya mfumo utakaowekwa na matumizi yake
• Kutoa taaluma ya utengenezaji wa majiko sanifu
• Kufanya majaribio ya  mifumo bora ya uzalishaji wa mkaa.
Kufuatilia maendeleo ya  mradi
• Ukusanyaji na uwekaji wa takwimu za mradi.
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.
Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja

Nafasi  # 4:  Afisa maendeleo ya majengo- Nafasi 1.
Habari:
Community Forests Pemba inahitaji, Afisa  wa Maendeleo ya Majengo ili kusaidia Jumuiya katika kazi za utengenezaji wa matufali ya udongo yenye kutumia saruji kidogo “Interlocking Compressed Stabilized Earth Block (ICSEB)”. Aidha, Afisa Majengo atatakiwa kusaidia na kutoa taaluma utengenzaji wa matufali ya bei nafuu kwa uenedelzaji wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa kutumia matufali hayo.

Sifa za muombaji:
1. Awe na Stashahada au shahada kutoka taasisi inayotambuliwa katika katika fani husika.
2.Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu katika uendelezaji wa majengeo ya bei nafuu.
3. Awe na ujuzi wa hali ya juu katika kufundisha na Mawasiliano
Majukumu:
• Kutoa mafunzo ya utumiaji wa mashine za (ICSEB) pamoja na ujenzi wa nyumba zake. mafunzo
• Kutoa mafunzo ya biashara na ujasiriamali.
• Kufuatilia ukuaji na maendeleo ya mradi
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.
Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja
 
Nafasi # 5: Bookkeeper and Clerical Assistant – nafasi 1
Community Forests Pemba (CFP) inahitaji; Mfanyakazi kwa ajili ya kazi za Uwekaji wa kumbu kumbu za mahesabu kwa kutumia Computer na  baadhi ya kazi nyengine. Mweka kumbukumbu za mahesabu atamsaidia Muhasibu kuingiza data, uwekaji wa kumbukumbu, kumbukumbu za matumizi ya afisi na mapato pamoja na “Data base”.
SIFA ZA MUOMBAJI
Awe amemaliza na kuwa na Cheti cha Diploma katika masuala “Computer on Financial Accounting” 
Uzoefu wa kazi hiyo usiopungua miaka miwili
Awe amemaliza katika Chuo kinachotambulika
Awe na uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiengereza na kuweza kuwafundisha wengine
Katika nafasi hii wasichana watapewa kipaumbele na wanashauriwa kuomba kwa wingi.
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.
Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja

Nafasi # 6: Dereva
Habari:
Community Forests Pemba(CFP) Inahitaji; dereva ili kusaidia katika shughuli mbali mbali za jumuiya.
Sifa:
• Awe na cheti cha ufundi wa kutengeneza magari
• Awe na uzoefu usiopungua  miaka mitatu katika kuendesha gari
• Awe na cheti cha udereva  kilichotolewa na taasisi inayotambulika.
Majukumu:
• Gari uwanja wa kiufundi na usimamizi wa wafanyakazi
• Kudumisha magari ya Jumuiya na kuyaweka katika hali nzuri
• Kufanya matengenezo ya magari pale yanapotokezea.
• Kueka kumbukumbu za masafa na utumiaji wa mafuta.
Muombaji atakaefanikiwa katika nafasi hii ni lazima kuwa na ujuzi wa mawasiliano ya kuandika na kuongea Kiswahili na kama atakuwa na uwezo wa kuongea Kiingereza atapewa umuhimu kwa vile atafanyakazi na watu wa ndani na nje ya Nchi.
Nafasi hii itakuwa na ufanisi mara moja

JINSI YA KUTUMA
Barua ya maombi yanatakiwa yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza pamoja na CV ya muombaji, na nakala za vyeti vyake.  Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Mei saa 11:30 asubuhi.  Wanawake wenye sifa watapewa kipaumbele. 
Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa mkono, kwa posta au kwa barua pepe kwenda anuani iliopo hapo chin:-
Mkurugenzi Mtendaji
Community Forests Pemba (CFP)
P.O. Box 177, Wete-Pemba
Minyenyeni - Pemba
Tel: +255 777 42 74 50
Email: cfp@forestsinternational.org
Web: http://www.forestspemba.org