Header

Katibu Mahsusi Daraja la III

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela anawatangazia nafasi mbalimbali za ajira kwa watanzania wote wenye sifa kama ifuatavyo:-

1. Katibu Mahsusi Daraja la III Nafasi 1

Sifa za waombaji:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kuteka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

Kazi na majukumu ya Katibu Mahsusi.
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa.
Kusaidia kutunza ·taarifalkumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safariza Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawakwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

Mshahara:- Ngazi ya mshahara TGS B

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/05/2015 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).
Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
Picha mbili (passport size) zilizopigwa hivi karibuni.

Aidha inasisitizwa kwamba:- .

Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania.
Wawe na umri kati ya miaka 18 - 45
Mwombaji ambaye hatazingatia maelekezo yaliyotolewa hapo juu, maombi
yake hayatashughulikiwa.
Maombi yote yawasilishwe kwa anuani ifuatayo hapa chini;

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA,
S.L.P 320,
KYELA.

Imetolewa na:-
C.R. Kasongo
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA