Header

Mtendaji wa Kijiji Daraja la III ( x 4)

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela anawatangazia nafasi mbalimbali za ajira kwa watanzania wote wenye sifa kama ifuatavyo:-

Mtendaji wa Kijiji Daraja la III Nafasi 4

Sifa za waombaji:-
Kuajiriwa wenye Elimu ya kidato cha nne (IV) au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahadalcheti katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Oodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. Kazi na majukumu ya Mtendaji wa Kijiji.

Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Kijiji.
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
Msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji.
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha
wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
kuongeza uzalishaji mali;
Kiongozi wa Wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji;
Kusimamia, kukusanyana kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji;
Mwenyekiti wa Kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji; na
Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

Mshahara:- Ngazi ya mshahara TGS B

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/05/2015 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).
Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
Picha mbili (passport size) zilizopigwa hivi karibuni.

Aidha inasisitizwa kwamba:- .

Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania.
Wawe na umri kati ya miaka 18 - 45
Mwombaji ambaye hatazingatia maelekezo yaliyotolewa hapo juu, maombi
yake hayatashughulikiwa.
Maombi yote yawasilishwe kwa anuani ifuatayo hapa chini;

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA,
S.L.P 320,
KYELA.

Imetolewa na:-
C.R. Kasongo
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA