Header

AFISA MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (Nafasi 10)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAN
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA JIJI MBEYA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Kwa mujibu wa Kibali chenye Kumb. Na. CB.170/364/01/G/49 cha tarehe 11 Machi, 2015 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya anatangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi husika kama ifuatavyo

NAFASI: AFISA MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (Nafasi 10)

Ngazi ya Mshahara – TGS B (345,000 X 930 Hadi 428,700/=)

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (IV) aliyehitimu mafunzo ya Astahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo

Utawala, Sheria, Elimu ya jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA
i. Katibu wa Kamati ya Mtaa
ii. Mtendaji Mkuu wa Mtaa
iii. Mratibu wa utekelezaji wa sera na sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa \
iv. Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu mipangi ya maendeleo katika mtaa
v. Msimamizi wa utekelezaji wa sharia ndogo pamo0ja na sharia nyingine zinanzotumika katika Mtaa
vi. Msimamizi wa utelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini katika Mtaa
vii. Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini katika mtaa
viii. Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote
ix. Mshauri wa kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama
x. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

MASHARTI YA UJUMLA
• Mwombaji awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Jiji la Mbeya
• Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai, kufukuzwa kazi, kuacha/kuachishwa kazi au kufungwa jela
• Maombo yote yaambatanishwe maelelzo na sifa binafsi zinanazojitosheleza (detail Curriculum vitae CVs) pamoja na namba ya simu ya mkononi
• Maombi yote yatumwe pamoja na nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya elimu (IV na VI) cheir cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni (Passport size) na iandikwe jina nyuma
• Testimonials”Provisional results” Statement of result” hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS HAVITAKUBALIWA)


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kupitia anuani hii

MKURUGENZI WA JIJI
HALMASHAURI YA JIJI
S.L.P 149
MBEYA, au yaletwe katika Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17/04/2015 saa 9 Alasiri