Header

Mtendaji Wa K1jiji

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama anatangaza nafasi Ishirini na saba (27) za kazi.
Maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo yanakaribishwa kutoka kwa Mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

MTENDAJI WA K1JIJI DARAJA LA III: NAFASI (3)

Majukumu:
Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji,
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa
Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kijijji.
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezajiwa Mipango ya maendeleo ya kijiji.
Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, Umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika Kijiji.
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote za Nyaraka za kijiji.
Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
Kupokea, kusikiliza na kutatua
Malalamiko na migogoro ya wananchi,
Kusimamia Utungaji wa sheria Ndogo za Kijiji na . Atawajibika kwa Mtendaji wa kata.

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) na;
Aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo.
Utawala, Sheria, Elimu ya jamii,
Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa
kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS B


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
Mwombaji awe raia wa Tanzania
Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nnej sita,
Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)Aidha maombi yatakayoambatanishwa na (Results Slip) hayatashughulikiwa.
Vyeti vyote vya Taaluma na kidato cha nnej sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili anayetambulika na Serikali.
Aidha uwasilishaji wa- taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
Watumishi waliopunguzwa kazijkufukuzwa kazi serikalini hawashauriwi kuomba, waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitisha barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya KiswahilijKiingereza.

Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayata fanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia
anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Kahama
S.L.P. 472, KAHAMA
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015, Saa 9:30 Alasiri.

Felix Kimaryo.
Mkurugenzi wa Mji
KAHAMA.