Header

Mtendaji Wa Mtaa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama anatangaza nafasi Ishirini na saba (27) za kazi.
Maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo yanakaribishwa kutoka kwa Mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III:
NAFASI (10)

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) na;
Aliyehitimu mafunzo ya Astashahada
Cheti katika moja ya fani zifuatazo:-
Utawala, Sheria, Elimu ya jamii,
Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA.
Katibu wa kamati ya Mtaa.
Mtendaji Mkuu wa Mtaa.
Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na
Halmashauri katika Mtaa.
Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu
Mipango ya Maendeleo katika Mtaa.
Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria
Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa.
Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama.
Msimamizi wa Utekelezaji wa mikakati
Mbali mbali inayohusu uondoaji wa
njaa na Umaskini katika Mtaa.
Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza
kumbukumbu za walipa kodi wote.
Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa na
Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

Ngazi ya Mshahara: TGS B
 
APPLICATION INSTRUCTIONS:

Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
Mwombaji awe raia wa Tanzania
Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nnej sita,
Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)Aidha maombi yatakayoambatanishwa na (Results Slip) hayatashughulikiwa.
Vyeti vyote vya Taaluma na kidato cha nnej sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili anayetambulika na Serikali.
Aidha uwasilishaji wa- taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
Watumishi waliopunguzwa kazijkufukuzwa kazi serikalini hawashauriwi kuomba, waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitisha barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya KiswahilijKiingereza.

Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayata fanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia
anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Kahama
S.L.P. 472, KAHAMA
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015, Saa 9:30 Alasiri.

Felix Kimaryo.
Mkurugenzi wa Mji
KAHAMA.