Header

Afisa Maendeleo Ya Jamii Msaidizi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama anatangaza nafasi Ishirini na saba (27) za kazi.
Maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo yanakaribishwa kutoka kwa Mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II NAFASI TANO (5)

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na, Mwenye cheti cha mafunzo katika fani ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Buhare na Rungemba au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali,

KAZl NA MAJUKUMU YA AFlSA MAENDELEO YA JAMII MSAlDlZI.
Kuratibu shughuli za maendeleo ya jamii katika Kijiji zikiwemo za wanawake na watoto na zikizingatia jinsia.
Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupaga, kutekeleza,
kusimamia na kutathmini mipango najau miradi yao ya maendeleo.
Kuhamasisha na kuwezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja
na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora vijijini,shule, zahanati, nk.
Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu nk.
Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa Viongozi wa
Kijiji na vikundi mbalimbali vya maendeleo Kijijini kuhusu:- Utawala
Bora, Uongozi, Ujasiriamali,mbinu shirikishi jamii nk ,
Kuwa kiungo kati ya Wanakijiji (Afisa Mtendaji wa Kata) na watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za Maendeleo.
Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea.
na kuratibu rasilimali zilizopo na kuzitumia katika miradi ya maendeleo.
kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo.
kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za Kijamii na,
Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI. '

Ngazi ya Mshahara: TGS B
APPLICATION INSTRUCTIONS:

Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
Mwombaji awe raia wa Tanzania
Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nnej sita,
Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)Aidha maombi yatakayoambatanishwa na (Results Slip) hayatashughulikiwa.
Vyeti vyote vya Taaluma na kidato cha nnej sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili anayetambulika na Serikali.
Aidha uwasilishaji wa- taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
Watumishi waliopunguzwa kazijkufukuzwa kazi serikalini hawashauriwi kuomba, waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitisha barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya KiswahilijKiingereza.

Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayata fanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia
anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Kahama
S.L.P. 472, KAHAMA
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015, Saa 9:30 Alasiri.

Felix Kimaryo.
Mkurugenzi wa Mji
KAHAMA.