Header

Katibu Mahsusi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama anatangaza nafasi Ishirini na saba (27) za kazi.
Maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo yanakaribishwa kutoka kwa Mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III NAFASI(5)

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV)
Awe amehudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.
Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet.E-mail na Publisher.

KAZl NA MAJUKUMU YA KATlBU MAHSUSl:
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
Kusaidia kutunza taarifa
kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tareje za vikao, safari za
Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zolizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu
Mkuu wake kwa wakati unaohitajika

Kusaidia kutafuta na kumpatia
Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokua amepewa na wasaidizi hao.
Kusaidia kupokeamajalada, kuyagawa
kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya,kuyatunza na
kuyarudisha sehemu zinazohusika.

Ngazi ya Mshahara:TGS.B
APPLICATION INSTRUCTIONS:

Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
Mwombaji awe raia wa Tanzania
Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nnej sita,
Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)Aidha maombi yatakayoambatanishwa na (Results Slip) hayatashughulikiwa.
Vyeti vyote vya Taaluma na kidato cha nnej sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili anayetambulika na Serikali.
Aidha uwasilishaji wa- taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
Watumishi waliopunguzwa kazijkufukuzwa kazi serikalini hawashauriwi kuomba, waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitisha barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya KiswahilijKiingereza.

Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayata fanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia
anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Kahama
S.L.P. 472, KAHAMA
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015, Saa 9:30 Alasiri.

Felix Kimaryo.
Mkurugenzi wa Mji
KAHAMA.