Header

Mtunza Kumbukumbu Msaidizi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama anatangaza nafasi Ishirini na saba (27) za kazi.
Maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo yanakaribishwa kutoka kwa Mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI

DARAJA LA II: NAFASI 4

Majukumu ..
Kutafuta kumbukumbu/majalada yanayohitajiwa na wasomaji wanaohusika.
Kudhibiti upokeaji , Uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka,
Kuweka majalada katika makundi
kulingana na somo husika kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka, n.k) katika majaIada.
Kudhibitiupokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/ nyaraka.
Kushughulikia Maombi ya kumbukumbu ya nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.

Mwombaji awe na sifa ziJuatazo:-
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha
Nne (IV) au cha Sita (VI)
Awe amehitimu mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu katika ngazi ya
Cheti katika mojawapo ya fani ya
Masjala kutoka katika vyuo vinavyo tambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS B'
 


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
Mwombaji awe raia wa Tanzania
Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nnej sita,
Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)Aidha maombi yatakayoambatanishwa na (Results Slip) hayatashughulikiwa.
Vyeti vyote vya Taaluma na kidato cha nnej sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili anayetambulika na Serikali.
Aidha uwasilishaji wa- taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
Watumishi waliopunguzwa kazijkufukuzwa kazi serikalini hawashauriwi kuomba, waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitisha barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya KiswahilijKiingereza.

Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayata fanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia
anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Kahama
S.L.P. 472, KAHAMA
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015, Saa 9:30 Alasiri.

Felix Kimaryo.
Mkurugenzi wa Mji
KAHAMA.