Header

Msaidizi Wa Kumbukumbu II & I - NAFASI 10

Mkurugenzi wa Manispaa ya lIala anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa
kama ifuatavyo:

Msaidizi Wa Kumbukumbu II & I - NAFASI 10
SIFA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IVNI wenye cheti cha Utunzaji Kumbukumbu kutoka chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
Wasaidizi wa kumbukumbu watafanya kazi zifuatazo hapa chini kwa kuzingatia fani walizosomea na
kazi wanazofanya ni kama vile Uhifadhi wa Nyaraka, Uhifadhi wa Kumbukumbu za Afya, Ardhi na
Masjala ya Kawaida,
1 KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II
Daraja hili la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya wasaidizi wa kumbukumbu
walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu
daraja la I.

2. KAZI ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA I
i. Kutafuta kumbukumbu/nyarakalmafaili yanayohitajiwa na wasomaji
ii. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
iii. Kuchambua, kuoredhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi
kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
iv. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjalalvyumba
vya kuhifadhia kumbukumbu.
v.Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika mafaili.
vi. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA - TGS. B
 
APPLICATION INSTRUCTIONS:

MASHARTI KWA UJUMLA

Mwombajilazima awe Raia wa Tanzania
Awe amehitimu na kupata Cheti cha Taaluma cha Kidato cha Nne (IV) NB. Results Slip hazikubaliki,
Awe na Cheti cha Kuzaliwa
Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo:-
i.Nakala za Vyeti vya Mwombaji vilivyothibitishwa,
ii. Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae),
iii. Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.
Kila Mwombaji lazima awe na Umri kati YCl miaka 18 - 45
Waombaji wenye sifa Pungufu au Zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba
kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.
Watumishi waliopunguza kazi/kufukuzwa kazi Serikali hawashauriwi kuomba
Waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitishia barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Barua ambato hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu.(i-iii) hazitashughulikiwa.
JINSI VA KUTUMA MAOMBI
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na
namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA VA ILALA
S. L. P 20950
DAR ES SALAAM:

TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI:-
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14105/2015 saa 9:30 Alasiri
Tangazo hili linapatikana pia kwenye Blog ya Manispaa ya lIala -
www.habariilala.blogspot.com
Limetolewa na;
ISAVA M. MNGURUMI
MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI VA MANISPAA VA ILALA