Header

TANGAZO LA KAZI UTUMISHI JAN 2014

Kumb. Na EA.7/96/01/E/27                                                               30 Desemba, 2013



TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 115 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:


MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.

ii.      Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.



vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

-       Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii.      “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

viii.      Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.      Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 13 Januari, 2013

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.        Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

xv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


1.0         DEREVA MASHUA/VIVUKO DARAJA LA II (FERRY/ BOAT OPERATOR GRADE II) - NAFASI 3

Nafasi hii ni kwa ajili ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)


1.1       MAJUKUMU YA KAZI

·         Kufunga na kufungua kamba za mashua/kivuko.

·         Kuchunga usalama nwa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/vivuko.

·         Kupanga abiria au magari kwenye mashua/kivuko.

·         Kuendesha na kuongoza mashua/kivuko.

·         Kutunza daftari za safari ya mashua/kivuko.

·         Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.

·         Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.

1.2       SIFA ZA MWOMBAJI

·         Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.


1.3       MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi



2.0     AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS OFFICER GRADE II) – NAFASI 3

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

2.1  MAJUKUMU YA KAZI

Hili ni daraja la mafunzo katika kazi hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Maafisa Kumbukumbu walio juu yake kwa cheo. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Afisa Kumbukumbu Daraja la I:-

·         Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza, na kusimamia matumizi ya kumbukumbu.

·         Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masjala.

·         Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, kutunza na kusimamia matumizi yake.


2.2  SIFA ZA MWOMBAJI

·         Kuajiriwa mwenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala,Kumbukumbu na Nyaraka kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

3.1     MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 15

3.1  MAJUKUMU YA KAZI

·         Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.

·         Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.

·         Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.

·         Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.

·         Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.

·         Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au wamepata idhni ya maafisa husika.

·         Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.

·         Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.

·         Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje. 

3.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa  wahitimu  wa  Kidato  cha  IV  waliofaulu  masomo  ya  Kiingereza,

Kiswahili na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu

kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
3.3
MSHAHARA

·         Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi



4.1     KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) – NAFASI 30

4.1  MAJUKUMU YA KAZI

·         Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.

·         Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.

·         Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.

·         Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.

4


·         Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

·         Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

·         Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

4.2  SIFA ZA MWOMBAJI

·         Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

4.3  MSHAHARA

·         Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.


5.1     MLINZI (SECURITY GUARD) – NAFASI 15

5.1  MAJUKUMU YA KAZI

·         Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.

·         Kuhahikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.

·         Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.

·         Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.

·         Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.

·         Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.

·         Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.


5.2  SIFA ZA MWOMBAJI

·         Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.


5.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.
5.4
MSHAHARA

·         Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.


6.1     MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (NYARAKA) DARAJA LA II – (RECORDS

MANAGEMENT ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 25 6.1 MAJUKUMU YA KAZI

·         Daraja hili ni la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Wasaidizi wa Kumbukumbu walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja I:-

·         Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.

·         Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.

·         Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

·         Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.

·         Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.

·         Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali

6.2  SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne (IV) au sita (VI) wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika fani ya Masjala.

6.3  MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi.


7.0     MSAIDIZI WA OFISI – NAFASI 22

7.1     MAJUKUMU YA KAZI

·      Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.

·      Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwsa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
·      Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
·      Kutayarisha chai ya ofisi.

·      Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
 ·      Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinastahili.

·      Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
·      Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
·      Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
·      Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.


7.2     SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.

7.3  MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.



8.0 MHANDISI DARAJA LA II - MAJI (WATER ENGINEER GRADE II) – (NAFASI 2)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Geita,

8.1    MAJUKUMU YA KAZI

·         Ujenzi na Usimamizi wa Vituo vya Hali ya Hewa, Vituo vya Upimaji wingi wa Maji mitoni (Discharge Measurements) na Uchukuaji wa sampuli za mchanga unaosafirishwa kwenye mito (sedment sampling) na kuzitafsiri.

·         Ukusanyaji wa takwimu kwenye vituo vya hali ya hewa na upimaji wa wingi wa maji mitoni na kuzitafsri takwimu hizo.

·         Kuandaa na kutayarisha Taarifa ya robo, nusu na mwaka mzima katika sehemu ya Haidrologia.

·         Kutayarisha kielelezo cha mtiririko wa maji ( Rating Curve Eqution )

8.2    SIFA ZA MWOMBAJI

·         Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

8.3    MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.


X. M. DAUDI


SECRETARY